Tujifunze kwa bidii ktk picha na ktk mifupa sura yake sehemu zake na eneo lake.
Tukiisha ya jua hayo tutavifahamu vizuio vingi vipatikanavyo wakati wa uzazi, kwa kuwa mtoto hulazimishwa kuputia ktk sehemu moja wapo nyembamba ya pango anapozaliwa.
Sura ya mifupa ya pango la nyonga
1. Mfupa wa pingili za nyonga upande wa nyuma ( the sacrum )
2. Mfupa wa kifandugu upande wa chini ( the coccyx )
3. Mifupa miwili ya nyonga kwa kila upandea ( the innominatebones )
1. Mfupa wa pingili za nyonga ni maendeleo ya uti wa mgongo zakaa ktk mfereji wake na zatoka ktk vitundu vyake. Mfupa huu umebonyea na watunga ukuta wa nyuma wa pango la nyonga kwa juu unagusana na pingili ya tano ya kiuno. Ukingo wake umechongoka kama nundu na unajibenua kwa ndani ya pango.
Nundu na unajibenu kwa ndani ya pango. Nundu hiyo yaitwa rasi ya nyonga.
Rasi hiyo ina maana sana wakati wa kuzaa, kwa sababu ikijitanua zaidi kwa ndani, eneo la mlango wa pango linapungua. Hivyo kichwa cha mtoto hupita kwa shida na pengine huzuiwa kabisa
2. Mfupa wa kifandugu ni maendeleo ya pingili za nyonga na mkia wa uti wa mgongo. Sehemu zake ni pingili 4-5 ndogo sana na zasaidia kufanya msingi wa pango.
Zanyoosheka zinapogusana na mfupa wapingili za nyonga.
Hivyo kichwa cha mtoto kinapopita hapa kinasukuma kifandugu kwa nyuma na pango hutanuka kiasi cha cm 1 hata 1.5
3. Mifupa miwili ya nyonga ni mikubwa,upo mmoja kila upande na yaungana kwa mbele. Ktk utoto kila mmoja una sehemu tatu zinazoungana ktk utu uzima, yaani wakati wa umri wa miaka 20.
Kila sehemu ina jina lake ndilo:
1. Kombe la kiuno ( the ilium )
2. Mfupa wa kinena ( the pubic bone )
3. Mfupa wa kukalia ( the ischium )
a. Makombe mawili ya kiuno ni mifupa mikubwa ya bapa na yafanana na bakuli kubwa pasipo msingi. Ukingo wake wa nje wapapasika chini ya mbavu kiunoni ( the iliac crest ) na waishilia kwa mbele na kwa nyuma kwa nundu.
Nundu za mbele za kiuno ( the anterior superior spines ) za papasika penye tumbo kwa juu ya kinena.
Nundu za nyuma za kiuno ( the posterior superior spines ) zapapasika mgongoni karibu ya pingili ya 4 ya kiuno. Kwa mbele makombe yaenea ktk mifupa y kinena.
Kwa ndani makombe yana ukingo uliovirigana ( the pelvic brim ) ukingo huu pamoja na mifupa ya kinena na mfupa wa pingili za nyonga watunga mlango wa pango la kweli.
b. Mifupa ya kinena ni midigo, myembamba na ya bapa. Hiyo ni ya panda nayo yaacha tundu ya kinena ndiyo itungayo sehemu ya mbele ya pango nayo imeunganishwa kwa kano shupavu ya mfupa ( symphysis ) ukingo wa chini ya mifupa hiyo umekunjika mfano wa uta ( the pubic arch )
c. Mifupa miwili ya kukalia ni minene tena butu nayo yafanya sehemu ya chini na ya nyuma ya pango.
Tukaapo twaitegemea. Kila mfupa wa kukalia una nundu nyembamba zielekeazo mbele kidogo nazo zapapasika kama miiba tuingizapo vidole ukeni ( the ischiatic spines )
Tulivyoona sehemu ya nyonga imekazwa katikati kwa ukingo kadiri ya kutunga mapango mawili.
Pango la juu lafanana na bakuli pana ndimo matumbo yakaamo, pia wakati wa uja uzito mimba yakaa humo. Ktk lile pango la chini ndimo vikaamo viungo vya uzazi, kibofu na mwisho wa utumbo mpana
Maoni
Chapisha Maoni