Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tukafuta taarifa zetu kama vile picha au hata video.
Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, teknokona inakuletea njia.
Sawa kama nilivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo urahisi uyafanye
__ Usihifadhi ( save ) kitu kingine chochote ktk simu kifaa chako au zima mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako
__ ( zima Wi-Fi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masahisho ( up date ) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike, kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafutaa
Tufahamu njia
Kama mafaili yako yapo katika memori kadi, ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya au hata kwa makusudi.
Kitu kina chofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB.
Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB ktk kompyuta haijionyesha ktk mfumo ule wa kuonekana kama umechomeka flash tuu.
Kama simu yako haifanyi hivyo na una uhakika taarifa zako hizo zilikuwa ktk sehemu ya memory kadi unaweza ukatumia adapta ya memori kadi hiyo na kuichomeka ktk kompyuta ili isome mafaili yaliomo ndani.
Sasa unaweza ukashusha programu ya Recuva ktk kompyuta ( unweza ukashusha ya bure au ya kulipia )
Bofya hapa kushusha Recuva
Ukishafungua Recuva kitu cha kwanza ni kuchagua mafaili gani unayofanya kuyafufua ktk kifaa chacho ( picha video nk ) unaweza ukachagua sehemu husikia ambapo unataka mafaili ya eneo hilo yafufuliwe.
Kitu cha muhimu cha kuweka akilini hapa ni kwamba programu ya Recuva itaonyesha maeneo ambayo inaweza fufua mafaili yaliyo futika tuu.
Mpaka hapo nadhani umekuwa mtaalamu juu ya jambo la kufufua vitu.
Fufua vitu vyako vya muhimu pindi tuu vinavyofutika kwa bahati mbaya.
Kwa kutumia njia hii huweza ukawa na wasi wasi kuwa utakuja kupiteza vitu vyako na usivipate tena.
Kama ukijatokeza hivyo unatumia Recuva
Maoni
Chapisha Maoni