Wanawake, watu wazima na vijana, watakao kazi ya ukunga wafahamu kuwa kazi yao yaheshimiwa sana wakiwa hodari na waaminifu.
Lakini wale walio dhaifu, wavivu, wenye akili ndogo au wafadhaikao upesi na kudharau. Sheria ya mungu, hawa hawafai hata kidogo.
Mkunga yampasa awe au ajibidishe kuwa na hali pamoja na tabia hizi
1. Awe na afya njema na hodari: Inamlazimu kukesha mara nyingi bila kulala.
Pengine ataitwa kwenda safari kwa miguu kusaidia wazazi mjini.
2. Awe na apende usafi na utaratibu: Kwake yeye mwenyewe na vitu atunzavyo. Avae nguo safi toka juu mpaka chini. Anawe hasa mikono na kusafisha kucha na kuzikata mara kwa mara .
Akiwamo katika chumba cha kupasulia ( operating Theatre ) Amwuguzapo mzazi aliyekwisha kuzaa akumbuke mafundisho kuwa. Baada ya kuzaa hubakia kidonda kikubwa ktk mji wa mimba, basi aangalie asiinhize vijidudu humo.
3. Awe mwenye akili na bidii:
Yaani apate kufahamikiwa na mafundisho na ajue kuyatumia, afahamu kuwa kusoma hakuna mwisho, aendelee kutaalamika kila anapoanfalia mara nyingi kwa akili kila namna ya uzazi, na ndipo apatapo ustadi.
Ni wajibu kwa mkunga kuangalia maendeleo ya uzazi, kumpima na kuandika habari za mzazi; aziandike na kuzisema habari halisi zisiwe za uwongo ay za ovyo ovyo. Inambidi vile vile kufahamu na kutambua upesi hatari za maisha ya mtoto na mama pia
4. Awe na moyo, mwenye huruma na upole: angalie mahitaji yote ya mzazi, kiu, jasho, haja, na kuchoka kwake.
Pasipo kuombwa, ampekinywaji; amkaushe jasho na kumnawisha au kumwogesha, ampe chombo cha haja kila ahitajipo. Mara kwa mara amtengenee mito na tandiko la kitanda, akimtegemeza vizuri mgonjwa. Asiwe mkali wala mwenye kukasirika pasipo sababu, akumbuke kuwa akiwa mpole atamtuliza mazazi, kila mara akumbuke mahangaiko na maumivu ya mzazi.
5. Awe shujaa: kwa kuwa atapata kuona mambo ya hatari yanayotisha ya maisha ya mtoto au mama mzazi. Kufadhaika, kulia na kukimbia hakuna faida. Lazima awe shujaa asaidie kwa kila namna na labda asingaliwapa msaada wangalikufa.
6. Amche Mungu na sheria zake: Twafahamu mimba ni kweli mtoto wa kibinadamu toka kuungana mbegu na kijiyai. Tena mimba si sehemu au kiungo cha mama kama mkono au tumbo. Aidha mfumo yawezekana ya kuwa damu ya mtoto haipatani na damu ya mama, bali na baba na kadhalika kwa ufupi mimba ni kiumbe kilicho mbali mbali na mama kuua mimba ni kumwua mtoto mchanga aliyekwisha zaliwa. Mkunga aheshimu maisha hayo ya mimba na kwa vyovyote vile asitoe msaada wa kuiharibu mimba, yaani kuitoa.
Mkunga aonapo kuhangaika na machungu mengi ya wazazi na pia furaha na upendo mwingi kwa watoto wao akumbuke baraka za ndoa; kuwa ktk ndoa wazazi hupata nguvu za kuwa na upendo huo na ikiwa yeye mwenyewe hajaolewa bado asijiachilie kuwa mkunga ataata baraka ya kazi zake akiwa mwenyewe anamcha mungu na sheria zake.
Asante sana kwa leo tunaishia hapa.
Maoni
Chapisha Maoni