Namna mtu anavyopenda kuonekana mbele ya wenzake huitwa mtindo wa maisha yake. Hata ikiwa mtu hatapenda aonekane mbele ya wenzake jinsi alivyo huo pia ni mtindo wa maisha yake.
Kuna mtindo ya maisha inayoweza kusababisha mtu aambukizwe magonjwa.
Vijana wengi hupenda kuonyesha mitindo gani ya maisha ?
Vijana wanapokuwa na mitindo hiyo ya maisha wanajisikiaje?
Mitindo hiyo ya maisha ya vijana huishia kwenye hali gani ?
Kumbe mitindo ambayo kijana hujisikia vizuri na maarufu huweza kugeuka kuwa ktk hali gani ?
Unafikiri ni mitindo gani ya maisha inaweza kusababisha mtu aambukizwe na magonjwa na kuwa na afya mbaya.
Kanuni za afya
Magonjwa ya kuambukiza huweza kukwepeka kwa kuzingatia kanuni za afya.
Baadhi ya kanuni za muhimu ni:
_ Kuoga kila siku kwa maji na sabuni na kuvaa nguo safi
_ kula chakula chenye virutubisho muhimu vya kujenga, kulinda na kutia mwili nishati na joto.
_ Kunywa maji safi na salama kila siku
_ Kuishi ktk nyumva iliyo safi ndani na nje
_ Mazingira yanayozunguka nyumba yawe safi
_ Kutumia choo kwa usafi na kuhakikisha watu wote wa familia wanatumia choo
_ Kuwa na mazoea ya kufanya kazi kwa kiasi siku na kucheza michezo tofauti
_ Kupumzisha mwili na akili kila wakati unapikuwa umechoka nk
Asante sana
Maoni
Chapisha Maoni