Watu wengi wanatamani kumiliki biashara siku moja na huenda wana mipango minzuri juu ya biashara zoa mipango hii inaweza ikwa vichwani tu au mingine ktk maandishi.
Lakini inapofikia wakati wa utekelezaji wa mipango hii ukosefu wa mtaji wa biashara hiyo ni kipingamizi kwa wengine
Lakini kuna jinsi kadhaa ambazo zinaweza kusaidia upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya biashara
Aina za mitaji
Kuna aina mbili ya mitaji kwa ajili y biashara au uwekezaji wa aina yoyote
__ Myaji wa mkopo
__ Mtaji wa mmiliki
Mtaji wa mkopo unakuwezesha kukopa toka kwa taasisi za fedha au mtu binafsi wa kiwemo ndugu jamaa na marafiki na kuhitajika kulipa ktk kipindi maalumu ikiwa pamoja na riba au bila riba
Aina hii ya mtaji inakuwezesha kufanya biashara lakini ni lazima uwe makini ktk utunzaji wa fedha zako na uzalishaji wake kwani mwishowe utahitajika kurudisha fedha zote pamoja na riba pengine kila mwezi.
Mtaji wa mmiliki ni mtaji toka kwa mtu au kampuni ambayo inahitaji kuwa na umiliki wa sehemu ya biashara. Hawa wanataka kupata faida kutokana na uwekezaji ktk kampuni au biashara yako.
Kama uko tayari kutoa sehemu ya umiliki wa biashara yako basi mtaji wa aina hii utakusaidia kuanzisha au kuboresha biashara yako.
Changamoto za kupata mitaji
Kupata mtaji wa biashara ni changamoto kubwa kwa wa jasiriamali kote duniani.
Japo fedha za mikopo zinapatikana ktk mabenki lakini biashara nyingi hazina miundo minzuri na mifumo ya fedha kuwezesha kupata mikopo.
Benki zimekuwa na masharti magumu sana kiasi kwamba biashara nyingi haziangalii huko kama sehemu ya kupata mikopo
Mikopo toka kwa ndugu na jamaa pia ina changamoto zake, si rahisi ndugu au rafiki akakuamini au akaamini kuwa biashara yako itafanikiwa, tunajua asilimia 90 za biashara zinazoanza zinakufa kila mwaka.
Maoni
Chapisha Maoni