Simulizi la uumbaji kwenye kitabu cha mwanzo ktk Biblia linasema kwamba adamu, mwanadamu wa kwanza, aliambiwa hivi na mungu: " matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula mpka ushibe.
Lakini kuhusu matunda ya mti wa ujunzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika" ( mwanzo 2:16,17 )
Maneno hayo yanaonyesha waziwazi kwamba iwapo Adamu angetii amri ya mungu, hangekufa bali angeendelea kuishi ktk bustani ya Edeni.
Kwa kusikitisha, badala ya kuchagua kutii ili aishi milele, Adamu aliamua kupuuza amri ya mungu na kula tunda alilokatazwa baada ya kupewa tunda hilo na hawa, mke wake. ( mwanzo 3:1,6 )
Madhara ya kutotii amri hiyo yanatuathiri sisi pia.
Mtume paulo alielezea hali hiyo hivi: " kupitia mtu mmoja dhambi iliingia ktk ulimwengu na kifo kupitia dhambi, na hivyo kifo kikaenea kwa watu wote kwa sababu wote walikuwa wamefanya dhambi, na hivyo kifo kikaenea kwa watu wote kwa sababu wote walikuwa wamefanya dhambi ( warumi 5:12 )
Bila shaka, " mtu [ Huyo ] mmoja ni Adamu.
Hata hivyo, alifanya dhambi gani, na kwa nini ilileta kifo?
Jambo ambalo Adamu alifanya. Yaani, kukataa kimakusudi kumtii mungu au kuvunja sheria yake, ni dhambi. ( 1 yohana 3:4 ) Na kama ambavyo mungu alikuwa amemwambia Adamu, adhabu ya dhambi ni kifo.
Ikiwa adamu na wazao ambao angepata baadaye wangeendelea kutii amri ya mungu,hawangekuwa na dhambi na kwa hiyo hawangepatwa na kifo.
Mungu hakuwaumba wanadamu wafe, bali waishi milele.
Kama Biblia ilivyosema hakuna shaka kwamba kifo " [ Kimeenea ] Kwa watu wote " lakini je, kuna sehemu fulani ya mwanadamu unayoendelea kuishi baada ya mtu kufa?
Huenda wengi wakajibu ndiyo, kwamba sehemu fulani inayoitwa nafsi, haifi.
Lakini hilo lingemaanisha kwamba mungu alimdanganya adamu. Jinsi gani?
Ikiwa sehemu fulani ya mwanadamu huendelea kuishi mahali pengine baada ya kifo, basi haingekuwa kweli kwamba kifo ni adhabu ya dhambi, kama mungu alivyomwambia adamu.
Biblia inasema: " mungu hawezi kamwe kusema uwongo." ( waebrania 6:18) Ukweli ni kwamba shetani ndiye aliyesema uwongo alipomwambia Hawa hivi: " Hakika hamtakufa." ( mwanzo 3:4 ) Hivyo basi swali ni; ni nini hutendeka mtu anapokufa?
Asante sana kwa uwepo wako.
Maoni
Chapisha Maoni