Inaweza kuonekana ni kitu cha kawaida lakini kuwa na furaha ya kweli na ya kudumu ni kitu ambacho kinatafutwa sana na watu wengi.
Ndio maana ukichunguza, harakati nyingi za kutafuta maisha zinalenga hasa kupata furaha, hata hivyo pamoja na watu wengi kuitafuta furaha sana, lakini bado wengi pia wanaendelea kugubikwa na huzuni ni kiwa na maana ni watu ambao wanaishi maisha hayana furaha sana kwa sehemu kubwa Je, hebu tujiulize ni mambo gani ambayo yanasababisha mtu mmoja akawa na furaha au mwingine akaikosa furaha majibu ya maswali haya utayapata kwenye makala haya. Kikubwa fuatana nami tuweze kujifunza pamoja.
1. Kufanya kazi usiyoipenda
Ipo asilimia kubwa sana ya watu ambao wanafanya kazi ambazo mara nyingi wanakuwa hawazipendi sana kwa lugha halisi wanakuwa ni watu wanafanya kazi ambazo hawazifurahii kikubwa kwao inakuwa ni kutaka kuingiza kipato tu, basi kama unafanya kazi ya namna hii ambayo huifurahii Lakini lengo lako ni kuingiza kipata basi elewa unabeba moja ya kitu ambacho kinakuzuia kupata furaha ktk maisha yako kwa namna moja au nyingine.
Watu wote wenye mafanikio wanafanya vile vitu ambavyo wanavipenda kutoka moyoni mwao, kama hufanyi kitu unachokipenda uwe na uhakika utaanza kujenga furaha yako
2. Kujilinganisha na wengine
Ni tabia ya wengi wetu tangu tukiwa watoto wadogo kutaka kujilinganisha na watu wengine. Kwa bahati mbaya tabia hii imekua ikikua hadi kuweza kufikia ukubwani na wengi wetu tena tumekuwa tukiindeleza pasipo hata kujua. Mara nyingi tumekuwa tukijilinganisha ktk vipato vyetu tumekuwa tukijilinganisha ktk mavazi na mambo mengine, uchungu nzima hivyo, hutokana na kujiinganisha huko sana imekuwa ikipelekea sisi kukosa furaha kikawaida huwezi kuwa na furaha kama kila wakati unajilinganisha na wengine.
Maisha na furaha yako inabaki kuwa yako kama kweli unaishi wewe kama wewe kujilinganisha na wengine ni sawa na kutengeneza mazingira ya kupoteza furaha yako moja kwa moja
3. Kuogopa mambo mengi
Ni asili ya binadamu kuwa na hali fulani ya woga kuna wakati tunakuwa tunakuwa tunogopa kujiingiza ktk jambo fulani, mathalani hata uthubutu wa kufanya kitu fulani, sasa inapotokea unakuwa ni mtu wa kuogopa sana mambo mengi na kila wakati, hiyo inakuwa ni changamoto moja wapo ambayo inakuzuia moja kwa moja wewe kuweza kupata furaha ya kweli, furaha ya kweli mara nyingi inapatikana hasa kwa wewe unapokuwa huru na mambo yako.
Unapokuwa huru huna hofu ya mambo mengi na kuishi kwa kujiamini hapo ndipo unakuwa na furaha ya kweli.
4. Kuishi wakati ulipita
Kuna watu ambao wengi wetu badala ya kuishi sasa, hujikuta ni watu wa kuishi kwa kukumbusha sana matukio mengi yaliyopita kama unaishi hivi kwa kukumbuka mambo mengi yaliyopita na ambayo yalikuumiza kwa namna moja au nyingine uwe na uhakika furaha yako utaipoteza.
Kujenga furaha ya kweli unatakiwa kuishi sasa na wala si kesho.
Fanya mambo yako kwa kuzingatia sana sasa watu wengi wenye mafanikio na furaha ya kweli wanaishi sasa na kusahau mambo mengine yaliyopita kumbuka wewe ndiye unayewajibika na kutengeneza furaha ya kweli wanaishi sasa na kusahau mambo mengi yaliyopita kumbuka wewe ndiye unaye wajibika na kutengeneza furaha ya kweli ktk maisha yako. Zingatia mambo hayo yanayokuzuia kupata furaha ya kweli
Maoni
Chapisha Maoni