Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mambo matano ya kuzingatia kama wewe ni mjasiriamali unayetaka mafanikio makubwa

Mafanikio ni kitu cha lazima sana ktk safari ya mjasiriamali uwe mjasiriamali mdogo wa kati au mkubwa kwa vyovyote vile unahitaji mafanikio. Lakini ili kufanikiwa na kufikia mafanikio hayo, yapi mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyazingatia. Mambo hayo ni kama haya yafuatayo

1.  Kujiwekea malengo

Ukiwa kama mjasiriamli unayetakiwa kufikia mafanikio makubwa, suala la kujiwekea malengo ni lazima kwako unapokuwa na malengo yanakuwa yanakupa mwelekeo sahihi wa kupata kile unachokitaka, Hiki ni kitu ambacho unahitaji kukizingatia sana kwani ni nguzo kubwa ya kufikia mafanikio makubwa

2.  Kujitoa Mhanga ( Take risks )

Hakuna mafanikio makubwa utakayoyapata ila kujitoa mhanga. Wajasirimali wote wakubwa ni watu wa kujitoa mhanga sana. Wanakuwa wako tayari kutoa kitu chochote ili mradi wafikie malengo yao. Kitu cha kuzingatia hata kwako wewe unalazimika kujitoa mhanga na kulipia gharama ili kufikia mafanikio makubwa

3.  Kutokuogopa kushindwa

Wengi wetu tumefundishwa sana kuwa kushindwa ni vibaya. Hali ambayo hupelekea tunakuwa tunaogopa kujaribu karibu kila kitu kwa sababu ya hofu ya kushindwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali unatakiwa kuwa jasiri na kujua kwamba mafanikio yanataka roho ya ujasiri na kutokuogopa kushindwa. Hayo ndiyo siri itakayokifikisha kwenye kilele cha mafanikio na sio uoga unaouendekeza

4.  Acha kurithika mapema

Ni kosa kubwa sana kujikuta unaridhika mapema eti tu kwa sababu ya faida unayoitengeneza sasa. Ni vizuri kujua safari ya mafanikio bado ni ndefu kwako, hivyo hutakiwi kuridhika kwa namna yoyote ile kama kuna Jambo umeifanikisha, endelea kwenye jambo lingine hadi kujenga mafanikio makubwa kabisa.

5.  Tafuta mentor

Acha kujidanganyai kuingia kwenye safari ya mafanikio huku ukiwa peke yako. Ikitokea umekwama kwa sababu huna mtu wa kukuelekeza au kukushauri huo ndiyo unakuwa mwisho wako. Hivyo ni muhimu kuwa na kiongozi wako " mentor " ambaye atakuongoza kwenye kufikia mafanikio yako. Kwa kuyajua mambo hayo yatakusaidia wewe mjasiriamali kuweza kuendelea mbele zaidi na kufanikiwa ktk safari yako yamafanikio

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.

Fahamu jinsi ya kutengeneza sabuni ya vyoo

Sabuni ya kusafisha vyoo Malighafi. 1. Sulphonics Acid Lita 1 2. Soda Ash nusu 1/2 kilo 3. Sless 4. Chumvi 1/2 kilo 5. Maji lita 17 1/2 _ 20 6. Rangi kijani 7. Pafyumu 8. Formalin Jinsi ya kutengeneza Weka maji lita 5 kisha anza kukoroga, ongeza lita 5 kisha lita 5 tena na mwisho lita 2 4. Chumvi 1/2 kg 3. Sless nusu lita 2. Soda ash nusu kilo 1. Sulphonics Acid lita 1 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu ni vinzuri kuweka kwenye ndoo lita 10 ya sabuni utaweka rangi kijiko 1 cha chai, rangi ya kijani pafyumu aina ya ' Rose two one ' au pino vijiko 5 vya chakula na Formalin vijiko 3 vya chakula. Formalin kwa ajili ya kuua wadudu ( bacteria ) ni vinzuri sana kuwemo kwenye sabuni ya chooni kwani ina kazi nyingi zaidi ya hiyo iliyotajwa Asante sana rafiki sasa chukua hatua ya kufanya hakika utafanikiwa sana

Somo: Roho mtakatifu Na mwl Christopher Mwakasege

Kushirikiana Na Roho Mtakatifu Anapotumia Moto kukuongoza ili utembee kwenye mapenzi ya mungu Biblia inafundisha ya kuwa wana wa mungu huwa wanaishi na wanatakiwa waishi kwa kuongozwa na roho mtakatifu ( warumi 8 : 14, 16, 17 ) Njia moja wapo anayotumia roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa mungu, ni kwa kutumia moto wa mungu anaokuja nao ndani ya mtu anapoingia kukaa kwake Biblia inasema juu ya yesu ya kuwa yeye atawabatiza kwa roho mtakatifu na kwa moto ( luka 3 : 16 ) na siku ya pentekoste, wakati wanafunzi wa kwanza wa yesu, walipokuwa wamekutanika pamoja kukuwatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao wote wakajazwa roho mtakatifu ( matendo 2 : 3,4 ) Unaposoma na kutafakari jambo lililotokea siku hiyo ya pentekoste, utajua kuwa kuna uhusiano kati ya ndimi za moto juu ya kila mmoja wao na kule kujazwa roho mtakatifu kwa kila mmoja wao ni dhahiri ya kuwa roho mtakatifu anaingia ndani ya kila mwana wa mungu akiwa pia na moto wa mungu pamoja nao kazi m...