Watu wengi wamezoea kuona au kutengeneza keki za unga na sukari. Lakini je, unafahamu kuwa kuna zaidi ya viungo hivyo.
Zipo keki za mboga na matunda na nyama.
Keki hii inaweza kutengenezwa kwa kutumuia nyama ya kuku, ng'ombe au mbuzi.
Kinachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha nyama unayotumia inakuwa ni ya kusaga isiyo na chembe ya mfupa.
Mahitaji
Unga nusu kilo
Siagi robo kilo
Chumvi nusu kijiko cha chai
Nyama ya kusaga robo tatu kilo mayai sita
Baking piwder kijiko kimoja cha chai
Viungo mdalasini, pilipili manga, tangawizi, vitunguu saumu, vitunguu maji kiasi
Namna ya kuandaa
Chukua viungo vyote vya upishi vinavyobidi kuoshwa hakikisha unachanganya.
Chunga unga na tia kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa siagi, halafu weka baking powder na mayai koroga mpaka ichanganyike.
Chemsha nyama viungo vyote isipokuwa vitunguu maji mpaka ikauke. Ipuka nyama na viungo vyote isipokua vitunguu vilivyokatwa vidogo vidogo paka siagi na tandaza unga, tia maji juu yake vuruga mayai yaliyobakia, mimina juu ya nyama csahanihk jiko la kuokea mpaka iive vinzuri, ipua na mimina ktk sahani wacha ipoe kata vipande tia ndani ya sahani
Tayari kwa kuliwa.
Maoni
Chapisha Maoni