Kuna wakati inakupasa uweze kuondoka kwenye jopo la watu ambao wanalalamika na kuingia kwenye kundi la watu ambao ni watu wasaka mafanikio daima na sio walalamikaji.
Kuna baadhi ya watu huelekeza mawazo yao hasi ktk kulaumu watu wengine kuliko kuwaza ni kwa jinsi gani wataweza kuyasaka mafanikio kiurahisi kabisa.
Mara nyingi sana tunatumia muda mwingi ktk kufanya mambo ambayo hayana manufaa ktk maisha yetu.
Kwa mfano, tumekuwa tukipoteza muda kwenye mitandao au kupenda mazungumzo yasiyo na msaada kwetu.
Kwa kuwa tunapoteza muda huo mwingi ktk mambo yasikuwa na tija inafika mahali tunakuwa ni watu maisha ya kawaida kila siku.
Na ili kutoka hapo kwenye kuishi maisha ya kawaida, hakuna dawa nyingine zaidi ya kuacha kufanya mambo yasiyo na manufaa kwetu.
Ukiweza kufanya hivyo, mafanikio utayapata tena kwa muda mfupi ipi kwenye kufanya mambo yenye manufaa kwako kila siku na si kinyume cha hapo
Najua unakuna kichwa unaweza daah sasa Afisa mipango kama ni kitaka mafanikio kwa muda mfupi nafanyaje tena kama ni hivyo na unataka kusikia jibu kutoka kwa afisa Benson nisikilize.
Ili kupata mafanikio kwa muda mfupi, mbali na kutokufanya mambo ambayo hayana manufaa kwako pia zingatia sana ya fuatayo.
1. Amini nguvu iliyopo ndani yako kwamba unaweza watu wengi hawaamini nguvu ambazo zipk ndani yao.
Wengi huamini ya kwamba mafanikio huja kwa watu mafisadi peke yao.
La hasha mafanikio yapo kwa kila mtu ambaye anamini ya kwamba yeye ni mshidi ktk maisha yake, bila kuangalia ni changamoto ngapi ambazo amezipitia
Unapokuwa unaamini uwezo na nguvu kubwa uliyonayo ndani mwako, inakusaidia sana kufikia mafanikio yako kwa muda mfupi kwa kadri utakavyozidi.
Kuamini na kutuma vipawa na nguvu zilizopo ndani yako utajikuta mambo mengi yanaenda vizuri tofauti na ulivyokuwa ukiwaza
Tumia muda sahihi, kufikia mafanikio yako.
Kuwa na kusudi maalumu kwa chochote anachotaka kufanya.
Moja ya changamoto ya watu wengi ambao walifeli kimaisha ni kwamba watu hao walifanya vitu bila kujua ni nini kusudio lao maalumu, hata hivyo ikawapalekea watu hao kuweza kuwa na malengo ambayo hayana tija.
Unakuta mtu anafanya biashara ukimuuliza kusudio la kufanya biashala hiyo utakushangaza ya kwamba hata mfanya biashara huyo huenda ukawa hajui pia.
Unahitaji kuwa na picha kamili ya jambo ambalo unalifanya kwa miaka ya mbeleni.
Picha hii ndiyo ambayo itakuonesha utaweza kufanikiwa kwa kiasi gani?
Au utashindwa kwa kiasi gani kama ni biashara ni lazima uwe na mlolongo mzima wa biashara ni lazima uwe na mlolongo mzima wa biashara yako jinsi itakavyokuwa kwa siku za mbeleni
3. Usichukue ushauri wa kila mtu
Kimsingi maneno ya watu yapo ambayo yanajenga kwa namna moja ama nyingine.
Ila maneno ambayo hajajengi ndiyo yapo mengi zaidi kwa mfano leo hii utakufanya biashara utakwenda kumshirikisha mtu ambaye yupo karibuni yako unakwenda kuomba ushauri, mtu huyo atakwambia biashara hiyo haifai mwishowe unajikuta unawabadilisha mawazo na kufanya jambo jingine na kwa kuwe wewe haujia amini unajikuta huna hata jambo hata moja ambalo unalifanya kwa uhakika.
Mwishowe unakosa hata jambo moja ambalo lina manufaa kwako.
4. Fany jambo la kwako
Ili kufanikiwa kwa muda mfupi ni lazima kujua wewe wako ndio siri ya mafanikio kwani moja ya watu wengi walioshindwa ktk maisha ni kwamba waling'ang'ana kufanya vitu visivyokuwa vya kwao ni kuache na swali la kujiuliza je jambo ambalo unalifanya ni lako pia kumbuka maisha ya mwanadamu yana fanana na miiba ya michongoma kwa maana ya kwamba kila wakati uwe tayari ktk kupambana na changamoto ambazo zinajitokeza kama ilivyo kwa miiba ya michongoma.
Maana miiba hii kila wakati upo tayari kwa ajiri ya upambanaji tu
Mwisho ni namaliza kwa kusema akili ikiamua kufanya jambo inawezekana hivyo ina hitajika nguvu ya mwili ktk kuisaidia akili ktk utekelezaji.
Naamini ukifanya mambo hayo yatakusaidia kufikia mafanikio yako kwa muda sahihi unaohitajika.
Maoni
Chapisha Maoni