Mafanikio makubwa huja kwa watu waliojiandaa. Kitu hicho ni baadhi ya watu wachache sana ambao hutmbua.
Watu wengi tunafikiri ya kuwa mafanikio tunayo yahitaji msingi wake mkubwa ni mtaji kwa maana ya kuwa na pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara au jambo lolote.
Ila ukweli ni kwa tayari kwa ajili ya mafanikio hayo kwani mafanikio huwa hayaji kwa bahati mbaya.
Kuwa na wazo hilo la kuwa na mtaji sio tatizo sana.
Ila tatizo linakuja pale ambapo tunasahau ya kuwa kuna tatizo kubwa ambalo linafanya.
Watu wengi washindwe kutimiza ndoto zao.
Jambo hilo ni woga binafsi hili ndilo tatizo kubwa ambalo watu wengi linawafanya washindwe kufikia ndoto zao.
Kuna usemi husema maisha ya mwanadamu yamethiriwa kwa kiasi kikubwa na woga.
Watu wengi wana woga wa uthubutu ktk jambo fulani mfano mtu leo hii anaweza ktk akili yake kwamba hawezi kufanya jambo fulani.
Akili yake ndivo inavyowaza hii ni kutokana na woga alio nao katika nafsi yake.
Woga binafsi mara nyingine hujenga na jamii ya watu ambao wanakuzunguka.
Mfano leo hii unataka kuanzisha biashara fulani kuna baadhi ya watu watakwambia hautaweza na wewe unaamini kweli hautaweza hivyo unaharisha kufanya jambo hilo, hii ni kutokana. Umeshajenga woga binafsi kwa kuwa mtu fulani alikwmbia hautaweza kufanya jambo fulani.
Wapo pia baadhi ya wazazi mara nyingi huwajenga picha mbaya watoto zao na watoto hao kuamini kuwa hawewezi.
Mfano mtoto wako kila siku anafeli ktk masomo yake.
Baadala ya wazazi kumuonesha njia za kuweza kufaulu.
Ila wewe unamkatisha tamaa.
Mwisho wa siku mtoto huyo anajenga woga binafsi, na kuamini yeye hawezi.
Ndugu msomaji wa makala hii inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa, hii ni kwa sababu kuna maneno ambayo uliambiwa na wazazi au ndugu wengine wanakuzunguka na leo hii bado unayakumbuka.
Mfano. Inawezekana uliambiwa wewe kichwa chako sio cha biashara na wewe ukayamini maneno hayo.
Hivyo wakakwambia ujikite zaidi ktk
Elimu yaani usome kwa bidii ili uje kuwa mtu fulani hapo baadae.
Kwa kuwa uliamini kuwa huwezi kufanya biashara na ukajikita ktk zaidi ktk elimu.
Umemaliza masomo yako, ajira hakuna kwa kuwa ulishaambiwa kuwa huna kichwa cha biashara leo hii unaona maisha yana zidi kuwa magumu na huna njia nyingine za kujiongeza ili uweze kufanikiwa.
Huwa ni ukweli usifichika wala hauhitaji mifano kutoka ulaya watu wengi tunashindwa kufanikiwa.
Hii ni kutokana na woga binafsi tulio nao watu wengi.
Wito wangu kwako ni kwamba ili uweze kufanikiwa unahitaji kujiamini, tumia akili, nguvu na kuwa na mawazo bora ya kufikiri yatakayokufanya wewe kutoka ktk hali uliyonayo kusonga mbele kuyasuka mafanikio.
Naomba kwa leo niishie hapa
Maoni
Chapisha Maoni