Tunaamini kabisa kwamba siyo siku zote huwa zinafanana mara nyingine siku huanza vema na kuendelea kwa furaha amani na mafanikio hadi mwisho wa siku hiyo mara nyingine siku yako huanza vibaya na kuishia vizuri.
Lakini ziko siku ambazo huonekana kuanza kwa mabalaa kama vile bahati mbaya, kupoteza vitu kuumia au huzuni ya moyoni na wengine hutabiri muonekano wa siku nzima kuanzia kwa yale yaliyojiri asubuhi.
Waswahili wamesema siku njema, huonekana asubuhi maana yake, mara nyingine hata siku mbaya pia hujionyesha ktk mawanzo wa siku hiyo.
Najua kuna baadhi ya imani zisizo rasmi ambazo hujaribu kulielezea suala hii mfano, ukiona bundi asubuhi au ukipishana na nyoka njiani.
Basi kuna walakini na siku yako hiyo.
Wapo wengine hasa wazungu ambao husema " ameamkia upande mbaya wa kitanda " sina uhakika kama kuna upande mbaya na mzuri wa kitanda.
Nia yangu ni kujaribu kukupa namna za kitaa laamu zinazoweza kukusaidia kuigeuza siku yako iliyoonekana kuanza vibaya kuwa nzuri na kupunguza pia uwezekano wa kuwepo kwa hizi siku zinazoaminiwa kuwa mbaya mswali
__ Je umewahi kukatishwa tamaa na kitu chochote mwanzoni mwa siku
__ Je umewahi kupoteza kitu mwanzoni mwa siku
__ Je umewahi kuumia moyo kwa kupata matarajio hewa ( disappointment ) mwazoni mwa siku au ktk siku fulani
__ Je umeshawahi kufanya kitu fulani na baadaye ukajutia kukifanya kitu na ukajihisi kushindwa au kuaibika
__ Umeshawahi kudhamiria kuingia kwenye uhusiano kwa matumaini yote na mara ukaona kila kitu kuwa ndivyo sivyo au umeshapitia matatizo fulani ya mwili, kama vile ugonjwa, ukilema ukaona labda ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yako.
Kama wewe ni mmoja wa watu hao basi karibu ktk ulimwengu wa wanadamu wa kawaida.
Wakati tunaposhindwa au kujihisi tumeshindwa mara nyingi tunadhani sisi peke yetu ndiyo tu wenye hali hiyo, ukweli ni kwamba, wengi hupitia huko na yamkini ktk hali ngumu zaidi
Kila fulani kila mmoja wetu amewahi kujutia jambo fulani alilolifanya kila mmoja wetu amewahi kukutana na magumu
Mambo ya kuzingatia
Jikubali kama mwanadamu wa kawaida na kwamba haistajabishi kushindwa yamkini unakata tamaa maana umezungumza na watu wanaoshinda na kufanikiwa tu
Angalia upande wa pili zungumza pia na waliowahi kushindwa .
Haijalishi ni muda gani ni kiasi gani ni ukubwa gani ni uzito kiasi gani wa magumu uliyopitia. Ninachojua ni kwamba inawezekana mimi na wewe kunyanyuka tena toka kushindwa kwetu, ndoto zetu zaweza kuwa kweli tena hii inategemea na kiasi uvumilivu wako
Tatizo siyo kushindwa kwa ukweli ni kule kushindwa kunyanyuka tena mara baada ya kushindwa mara ya kwanza Angalia mchezo wa ngumi, haijalishi mtu anapigwa na kuanguka mara nyingi kiasi gani, lakini pale anaposhindwa kunyanyuka ndiyo refa hutangazwa KNOCK OUT yaani ameahinda kabisa
Ili kuweza kunyanyuka tena
Jikubali kama mwnadamu wa kawaida tambua kushindwa kupo na ni moja ya matukio ya maisha yetu
Unapoanguka chini, jitahidi usibaki chini ( tofautisha kuanguka kwa mtoto na mtu mzima ) fahamu kushindwa kwa kweli ni kule kushindwa kunyanyuka mara baada ya kuanguka .
Jifunze, pata shule kupitia mapito na magumu unayoyapitia tatizo pia siyo kufeli, bali ni kufeli kujifunza ktk kule kufeli. Kufanya kushindwa kwako kuwe kama mawe ya kukanyagia ktk kuvukia kwenda upande wa pili.
"Tutakushangaa, ukiangushwa na jambo lile lile linalokuangusha mara zote"
Jifunze kutumainia ktk imani uliyonayo imani ni injini isiyoshindwa ktk suala zima la kushindwa na kuweza.
Imani huwa poozeo kwa maumivu tunayoyapitia
__ Jitahidi, vuta zaidi kazana amini kuwa kitu chema cha weza kutoka ktk mikono yako midomo yako, moyo wako au hata mawazo yako.
Asante sana kw leo tunaishia hapa
Maoni
Chapisha Maoni