Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Aina 03 za wanaume ambao wake zao wanakereka kuwa nao

1: wanaojiona kama wafalme ( king husband )

Hii ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa.
Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutuma tuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosa kidogo ni maneno au kipigo mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

2: Wanaume wanaojihisi Bado hawajaoa ( Bacher husband )

Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha.
Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote ktk ndoa yake.

3: Wanaume wenye Gubu ( Acidic Husband )

Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya msingi mambo hayaishi kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirika leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyingi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.

Utengenezaji wa sabuni

1: Utengenezaji wa sabuni za mche     Malighafi: 1: Caustic kg 4 2: Maji lita 10 3: Mafuta lita 20 4: Sodium Silicate Kg 2 5: pafyumu mili lita. 250 __  300 6: Chumvi vijiko 2 vikubwa Sabuni hii unaweza kuogea na kufulia inakuwa nzuri sana. Jinsi ya kutengeneza Loweka Caustic kg 4 kwenye maji ya lita 10 kwa siku 3. Ndani ya siku hizo tatu, utakuwa ukikoroga kila siku asubuhi na jioni kwa dakika 5. Kisha chukua sodium silicate kg2 ikifuatiwa na chumvi vijiko 2 vya chakula na mafuta huku unaendelea kukoroga kwa juhudi. Baada ya hapo weka kwenye maumbo kwa siku 3 __ 5 ili igande vizuri. Asante sana rafiki

Fahamu jinsi ya kutengeneza sabuni ya unga

Sabuni ya unga Malighafi. A. Solphonic lita 1 B. Sodium sulphate kilo 3 C. Optical brightener vijiko 10 vya chakula D. Nausa vijiko 10 vya chakula E. Soda ash kilo 3 F. Pafyumu kijiko 1 cha chakula G. Rangi kijiko 1 cha chakula Jinsi ya kutengeneza Andaa malighafi kwa resho kama ilivyoandikwa hapo juu, Beseni na mwiko, kisha weka kimoja kimoja ukianza na herufi A __ G, huku ukikoroga mseto wako kwa muda wa dakika 15 halafu anika sehemu yenye hewa kivulini hadi ikauke. Hapo sabuni yako ya unga itakuwa tayari, iweke kwenye vifungashio ipeleke aokoni