Kila tatizo lina chanzo chake hakuna tatizo linatokea kwa bahati mbaya na ukifanikiwa kujua chazo utafanikiwa kutafanikiwa kutatua tatizo kwa asilimia mia moja.
Kwenye kushughulika na tatizo kuna namna ambayo unaweza kufanya namna ya kwanza unaweza kuondoa tatizo au kuongeza tatizo kutokana na njia uliyotumia ili kutafuta tatizo.
( luka 6:17,19 ) Akashuka pamoja nao akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi na makutano makubwa ya watu waliotoka uyaudi wote na yerusalemu na pwani ybTiro na sidoni, waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu waliponywa na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.
Baadhi ya vyanzo vya matatizo ni
UCHAWI Ni chanzo cha matatizo kutokana na baadhi ya watu kufanya uchawi na biblia imeongelea kwa habari ya kulogwa.
Mungu hapendi uchawi ( wagalatia 3:1 ) Enyi wagalatia msio na akili ni nani aliyewaloga ninyi ambo yesu kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa
Roho ya kukataliwa
( 1 mambo ya nyakati 4:9,11 ) Naye yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze na mamaye akamwita jina lake yabesi akisema Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.
Huyu yabesi akamlingana mungu wa israeli akisema au kwamba ungenibarikia kweli kweli na kunizidishia hozi yangu na mkono wako ungekuwa pamoja nami nawe ungenilinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu naye mungu akamjalia hayo aliyoyaomba naye kelubu, nduguye shuha, akamzaa mehiri aliyebkuwa Babaye Eshtoni
Roho ya kukataliwa ni chanzo cha matatizo ndiyo maana yabesi akamlingana mungu.
Chanzo kingine ambacho ni
Mashetani au mapepo wachafu
( luka 6:18,19 ) Na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu waliponywa
Kuna waru wana sumbuliwa na mashetani mapepo majoka ndio wanasababisha shida na matatizo mbalimbali mashetani ni malaika wachafu ambao walitupwa kutoka mbinguni na wapo duniani ili kufanya shughuli za kishetani
(ufunuo wa yohana 12:7,10 ) Kulikuwa na vita mbinguni mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake nao hawa kushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ukitaka kumtoa pepo mchafu ni lazima ushindane kwa kutumia mamlaka ya jina la yesu na damu ya yesu.
( waefeso 6:12 ) Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama Bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya ktk ulimwengu wa roho.
Usianze kuwaza kupata ufumbuzi wa tatizo lako ukakaa na kusema Bwana anajua.
Je umefanya nini kwa ajili ya Bwana ili na yeye afanye kwa ajili yako.
Kuna malaika wa tatu ambao ni lusifa, Gabrieli na michaeli.
Lusifa / kerubi / shetani / Alikuwa kwenye kitengo cha sifa mwingine Gabrieli huyu ni malaika wa taarifa.
Tunaona malaika Gabrieli alikwenda kwa Elizabeth.
Pia alimtoke Danieli alipokuwa amefunga akamletea taarifa.
Kuna malaika mwingine anaitwa michaeli huyu ni malaika wa vita ambaye ana malaika wengine wapo chini yake.
Tunaona kuwa chanzo cha matatizo kimeanza kwa kiumbe mmoja ambaye alitupwa hapa duniani aitwaye shetani.
Biblia inatupa uhakika kuwa shetani yupo na mapepo wanafanya kazi chini yake.
( isaya 14:12,15 ) Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni Ewe nyota ya affajiri mwana wa asubuhi jinsi ulivyokatwa kabisa Ewe uliyewaangusha mataifa Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Ni takiinua kiti changu juu kuliko nyota za mungu, Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano ktk pande za mwisho za kaskazini Nitapaa kupita vimo vya mawingu nitafanana na yeye aliye juu lakini utaahushwe mpaka kuzimu mpaka pande za mwisho za shimo.
Kuna vitu ambavyo huwa vinasababisha shetani awe na nguvu kwenye maisha ya watu.
Mafano unapokuwa unaishi maisha ya dhambi usitegemee utamshinda shetani kirahisi ama kama una maagano ya ukoo yatokanayo na mazindiko ni vigumu sana kumshinda shetani aliyeshikilia sehemu ya maisha yako. ( yohana 10:10 ) ( luka 10:19 ) ( yakobo 4:7 ) ( 1 wathesalonike 2:18 ) ( mhubiri 9:11 )
Malaika ni Roho lakini wanaweza kuvaa miili ili kutimiza kusudi fulani unaweza ukaona Dada mzuri anapendeza au kaka mzuri hana makuu ni mtaratibu kumbe ni malaika wa giza amevaa mwili anakutega tu ili aharibu hatima ya maisha yako. ( 2 wakorintho 4:4 ) soma.
Unaweza kuona kumbe shetani / lusifa ni malaika ambaye alikuwa mbinguni baada ya kutupwa Duniani akaanza kufanya shughuli zake hapa Duniani akiwa pamoja na mawakala wake.
Lakini sisi tulio ndani ya yesu hana kitu kwetu tuna weza kumshinda kama alivyoshindwa mbinguni.
Hakuna binadamu, shehe, imamu, padri ambaye alikwenda kuandaa mahali mbinguni.
Bali ni yesu kristo peke yake ndiye aliyekufa msalabani na akatuambia anakwenda kutuandalia mahali.
Kuzimu inaweza kuvaa mwili kama binadamu, unashangaa unakutana na mtu ana kwambia mfanye ubia mfanye biashara pamoja kumbe nia yake inakuwa ni kuharibu biashara yako na kukuibia nyota yako mtu anakwambia muwe kitu kimoja kwenye jambo fulani kama haupo vinzuri kiroho utaishia kuibiwa Baraka zako na kubaki na magonjwa na balaa kwenye maisha yako.
( 2 wakorintho 11:14,15 ) soma
Shetani anaweza kujigeuza kuwa kama malaika wa nuru lakini mwisho wake ni kuharibu hatima ya maisha yako. ( 1 petro 5:8 ) soma.
Petro ametufundisha tuwe makini usikae tu uko mzembe mzembe uwe mpole kama ua mjanja kama nyoka kwa sababu shetani kila siku anatafuta mbinu mpya ili akuzuie usitimize kusudi lako.
Ni vinzuri uwe Baba wa kiroho ili kuunganishwa na madhabahu ya mungu usiwe mtu wa kuhamishwa hamishwa siyo leo uko kw Nabii kesho kwa mtume unakuwa mtu asiye na makao unajikuta unabaki kujenga tumaini kwenye maji ya Baraka, sabuni za upako, vitambaa asali na mambo kama hayo wakati damu ya yesu ipo na neno lake na jina lake vilitolewa tena wala haina tarehe ya kusema imeisha muda haifanyi kazi.
Mambo ambayo hayampendezi mungu yanampa shetani nafasi ya kuwa na nguvu kubwa kwenye maisha yetu ila kama ukikaa vinzuri na mungu shetani hana uwezo alishindwa mbinguni na sisi tuna mamlaka ya yesu kristo kumshinda hapa duniani.
( waefeso 4:27 ) ( luka 22:3 ) ( waamuzi 6:11-12-13) ( waamuzi 21:22,25 )
Kwenye gamilia mtu anaweza kushindwa kuchomoza kwenye familia mtu anaweza kushindwa kuchomoza kwenye mafanikio kwa sababu ya wachawi mchawi anaweza kuwa Baba au mama au mtu yeyote ndani ya familia
Gidion alishindwa kwa sababu ya uchawi wa Baba yake vivyo hivyo kwenye maisha yetu kuna watu wanafunga hawali ili maisha ya mtu yaharibike.
Gidioni tangia. Kuumbwa kwake aliubwa kuwa shujaa lakini uchawi wa Baba yake ulimzuia asidhihirishe ushujaa wake.
Kila mtu unayemuona ana kusudi lake hapa duniani.
Lakini kuna vitu vimezuia kusudi lisitimie kuna sababu kwa nini unapitia hayo unayoyapitia simama kwa maarifa ya vyanzo hivi haribu madhabahu zilizoiba nyota yako na kukulaza utafanikiwa kwa jina la yesu.
Hautakiwi kuomba ili mungu akupe kwa sababu mungu alishakupa tayari lakini wapo wanaozui mazingira ya uchawi au ushirikina ya kiwepo yana shika kile kitu ambacho umepewa.
Simama kama askari wa yesu pigana vita vya rohoni utapenya kwa jina la yesu amen
Mara nyingi mtu anaweza kuwa na kitu cha kishetani ndani yake ndicho kinacho haribu maisha yako bila wewe kujua.
Kuna watu mashujaa lakini wamechoka kwa sababu ya madhabahu zilizo washikilia zikibomolewa mtu anaanza kung'aa.
Unapobomoa madhabahu za kichawi ndipo wanapoanza kukutafuta ili kukurudisha kwenye mazindiko.
Njia nyingine ni kumwendea mganga wa kienyeji.
Njia nyingine ambayo inasababisha mapepo kuingia ndani ya mtu ni mavazi.
Kuna mavazi ambayo ni utambulisho unaweza kukuta mtu kuvaa tshirti ina macho ya mtu kumbe anajiunganisha na zile tamaduni za watu wale bila yeye kujua.
Mavazi ni muhimili mkubwa wa mashetani kumwiingiza mtu, Mti anaweza kunuizia kitu kwenye mavazi akakupa ukavaa kikawa ndio chanzo cha matatizo kwako.
( Ezekieli 13:18,19 ) useme, Bwana mungu asema hivi ole wao wanawake wale washonao hirizi ktk viungo vyote vya mikono wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo ili wawinde Roho za watu je mtaziwinda Roho za Watu wangu na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe
___ Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate ili kuziua roho za waru ambaobhaiwapasi kufa na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
____ Mavazi yanaweza kubeba roho zikamwingia mtu, mavazi yanaweza kubeba nguvu za mungu ( matendo ya mitume 19:12 ) soma
Eliya alipoondoka alimwachia Elisha vazi naye Elisha alipolivaa tu upako mara mbili
Njia nyingine ni wivu na tamaa
Wivu na tamaa vinaweza kuwa ruhusu mashetani kuingia ndani ya mtu ( matendo ya mitume 10:38 ) ( mathayo 9:35 ) ( mathayo 14:17 ) ( marko 6:7 ) ( marko 16:17,18 ) soma
Tukimwamini yesu rumepewa leseni ya kuwa toa pepo ( 2 wakorinrho 10:5 ) soma.
Maarifa ni ya muhimu ili tuyatumie kushambulia kupiga ili tumiliki kile tunachotakiwa kumiliki kwa jina la yesu. Amina
Maoni
Chapisha Maoni