Jinsi Roho Mtakatifu Anavyomuongoza Mtu, kwa Kutumia Moto Wa Mungu
Moto wa mungu unapowaka ndani ya moyo wa mtu ukiwa umebeba taarifa ya ghadhabu na maonyo ya mungu.
Tunasoma katika ( Isaya 66:15 ) Ya kuwa maana Bwana atakuja na moto ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao na maonyo yake kwa miali ya moto.
Bwana atakuja na moto ina maana ya mungu kujifunua kwa njia ya au kwa ishara ya moto na ktk kujifunua huko ndani ya moto huo kuna ujumbe au taarifa ya malipo ya ghadhabu yake na maonyo yake kwa tafsiri iliyo rahisi utaona ya kwamba moto wa jinsi hii.
Unapowaka moyoni mwako ni kwa ajili ya kukupa onyo ya kuwa kuna jambo lililomkasirisha mungu na lina adhabu inayokuja kama malipo ya kosa hilo na ili ujumbe wa moto huu wa mungu unaokuja kwa jinsi hii yaani uliobeba ghadhabu yake na maonyo yake uwezo kueleweka huwa hauji pekee yake.
Moto wa jinsi hii utawekwa na kudhihirishwa ndani ya moyo wa mtu na Roho Mtakatifu
Roho mtakatifu ataambatanisha moto huu pamoja na hofu ya mungu na huzuni ya mungu na maombolezo na kukunyima amani ya kristo moyoni na au kukukosesha raha nafsini.
Hofu ya mungu inapoambatana na moto wa mungu moyoni mwa mtu ni ujumbe toka kwa Roho Mtakatifu ya kuwa moyo na mtu huyo usije ukadharau onyo hilo la ujio wa ghadhabu ya mungu.
Na unapoona hofu ya mungu ikiwa imeambatana na moto wa mungu unaona pia vimeambatana na huzuni ya mungu na hali ya kuomboleza moyoni au hali ya kukosa amani au hali ya kukosa raha ujue ni roho mtakatifu anakujulisha ya kuwa pamoja na kwamba ghadhabu ya mungu inakuja.
Lakini inawezekana ikaepushwa kwa njia ya mtu kukubali maonyo na kutubu.
Hili tunalipata tunaposoma kitabu cha ( wakorintho 7:10 ) Ya kwamba maana huzuni iliyo kwa jinsi ya mungu hufanya toba liletao wokovu lisilo na majuto.
Hivi ndivyo pendo la mungu linavyofanya kazi, mungu anapoghabika kwa sababu ya kosa la mtu Roho Mtakatifu anampa mtu huyo taarifa ya ghadhabu hiyo lakini pia na onyo ambalo akilitii na kutubu ghadhabu ya mungu inafutwa na kuondolewa.
Fahamu jambo hili ya kuwa Roho Mtakatifu anaweza kumuongoza mtu kwa jinsi hii
____ Kwa ajili ya mtu huyo mwenyewe
___ Au kwa ajili ya mtu mwingine ili apewe hiyo taarifa na kuombewa
____ Au kwa ajili ya eneo kama mji au kijiji au kitongoji au nchi ili liombewe.
Amin
Maoni
Chapisha Maoni