Kwa kuwa dunia inayotajwa hapo inatamaa ambazo mungu anashutumu, ni wazi kwamba si dunia halisi Ni wanadamu wanaompuuza mungu na jambo hilo linawafanya kuwa adui zake ( yakobo 4:4 ) wanadamu hao " watahukumiwa adhabu ya uharibifu wa milele " ( 2 wathesalonike 1:7,9 ) kwa upande mwingine watu wanaotii agizo la yesu kristo la kuepuka kuwa " sehemu ya ulimwengu " wanatumaini la uzima wa milele ( yohana 15:19 )
Andiko la ( 1 yohana 2:17 ) linamalizia hivi " yeye anayefanya mapenzi ya mungu anadumu milele " ndiyo mtu huyo atakuwa na tumaini la kuishi milele hapa duniani, kwa kuwa andiko la ( zaburi 37:29 ) linasema hivi " waadilifu wenyewe wataimiliki dunia, nao watakaa milele juu yake "
" Msiwe mkiupenda ulimwengu au vitu vilivyo katika ulimwengu. Yeyote akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo ndani yake "
Mwisho wa dunia utakuja Jinsi gani
Mwisho utakuja kupitia hatua mbili kuu, kwanza mungu ataharibu dini ya uwongo, inayofananishwa na kahaba anayeitwa Babiloni mkubwa ( ufunuo wa yohana 17: 1,5/ 18,8 ) ingawa anadai kuwa mshikamanifu kwa mungu amekuwa huu. Hata hivyo, viongozi hao watamgeuka " watamchukia yule kahaba na kumfanya kuwa ukiwa na uchi nao watakula sehemu zake zenye nyama [ au utajiri ] na kumteketeza kabisa kwa moto ( ufunuo 17:16 ) pili, mungu ataelekeza fikira zake kwa viongozi hao wa kisiasa " wafalme wa dunia nzima inayokaliwa " wataharibiwa pamoja na watu wote waovu katika " vita vya ile siku kuu ya mungu mweza yote " ambayo pia inaitwa " Har magedoni ( ufunuo 16: 14,16 )" mtafuteni yehova, ninyi nyote mlio wapole wa dunia utafuteni uadilifu utafuteni upole. Huenda mkafichwa katika siku ya hasira ya yehova ( sefania 2:3 ) amina.
Maoni
Chapisha Maoni