Simulizi la uumbaji ktk kitabu cha mwanzo linasema hivi yehova mungu akamfanya mtu kutoka ktk mavumbi ya inchi na kupuliza ktk mianzi ya pua yake pumzi ya uhai, naye mtu akawa nafsi hai usemi " nafsi hai " unatokana na neno la kiebrania " ne phesh " linalomaanisha kiumbe anayepumua ( mwanzo 2:7 ) Hivyo, Biblia inaonyeaha waziwazi kwamba mwanadamu hakuubwa akiwa na nafsi isiyoweza kufa. Badala yake kila mwanadamu ni " nafsi hai " Hiyo ndiyo sababu hakuna andiko ktk Biblia linalotaja kuhusu "nafsi isiyoweza kufa " Ikiwa Biblia haisemi kwamba wanadamu wana nafsi isiyoweza kufa kama wengine wanavyodai, kwa nini dini nyingi hufundisha jambo tofauti ? Misri ya kale inatoa jibu la swali hilo
JE WANADAMU WANAWEZA KUISHI MILELE
Miaka michache iliyopita, watafiti waliripoti kugunduliwa kwa mimea fulani inayoota chini ya maji wanayoamini imeiahi kwa maelfu ya miaka, huenda muda mrefu kuliko kiumbe kingine chochote duniani. Mimea hiyo ni ya jamii ya posidonia oceanica, aina fulani ya nyasi zilizoenea kwenye sakafu ya bahari ya mediterania kati ya Hispania na saiprasi. Ikiwa mimea inaweza kuishi kwa miaka mingi hivyo namna gani wanadamu ? Baadhi ya wanasayansi ambao huchunguza suala la uzee wanahisi kwamba kuna uwezekano wa kuongeza muda wa kuishi kwa mfano kitabu fulani kuhusu suala la uzee kinasema kuwa kinachunguza kwa kina " Maendeleo makubwa ya kisayansi " ktk nyanja hiyo hatujui ikiwa maendeleo ya kisayansi yatakuwa na mchango wowote ktk kongeza muda wa kuishi wa mwanadamu au la. Hata hivyo, tumaini la kweli la kuishi milele halitegemei sayansi. Biblia inatuelekeza kwa muumba wetu yehova mungu, na kusema hivi " kwako wewe iko chemchemi ya uzima ( zaburi 36: 9 ) Yesu kristo alisali hivi kwa mungu " Uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, mungu wa pekee wa kweli, na juu ya yule uliyemtuma yesu kristo ( yohana 17: 3 ) Kwa kweli jitihada zetu za kumjua na kumendeza yehova mungu na mwana wake yesu kristo, zitathawabishwa kwa baraka za milele.
Maoni
Chapisha Maoni