Rafiki yangu mmoja aliniandikia jana akitaka kujua huyu Bezos hasa ni nani na amewezaje kumpiku mtu tajiri duniani Bill Gates.
Hapa ndipi niligundua wapo wengi hawajawahi kumsikia au kumjua kwa undani Jeff Bezos
Nimekuandalia makala hii yenye mambo saba muhimu ambayo huenda huyajui kuhusu tajiri huyu mpya namba moja duniani yapo mengi ya kujidunza kupitia maisha yake .
1: utoto wake ulikuwa na changamoto:
Mama yake mzazi alipata mimba akiwa shuleni. Baadaye aliolewa na aliyempa mimba lakini waliachana kutokana na maisha kuwa magumu na mwanaume kuwa mlevi.
Baadaye aliolewa na mwanaume mwingine ambaye alimchukulia jeff kama mtoto wake wa kumzaa. Mpaka anafikisha miaka 10
2: Biashara yake kuu ni Amazon
Bezos ni mwanzilishi wa mtandao mkubwa wa kuuza vitu wa Amazon. Ni mtandao ambao ulianza kwa kuuza vitabu, ila kwa sasa unauza kila kitu mtandao huu ulianza tangu mwaka 1994 na umekuwa unakua kwa kasi kubwa kila mwaka.
Kampuni hii alianzia nyumbani kwake alipokuwa anaishi.
3: Amewahi kuwa mhudumu wa mgahawa:
Hakiwa kijana mdogo, Bezos amewahi kuwa mhudumu wa mgahawa wa mc Donald's akiwa kama mhudumu na msafishaji wa meza.
Anasema kazi hii ilimpamsingi muhimu sawa wa kubeba majukumu yake.
4: Aliacha kazi inayolipa kwenda kujijiri
__ Kabla ya kuanzisha Amazon, Bezos alikuwa ameshaajiriwa sehemu tatu, Firel, Bankers Trust company na D.E shaw, zote zikiwa kampuni zinazo hususika na fedha na uwekezaji. Ktk kampuni ya tatu, aliweza kupanda vyeo mpaka kufikia nafasi ya makamu wa rais wa kampuni hiyo, tena ktk umri mdogo sana.
Wakati anaacha kazi yake na kwenda kujiajiri, kila mtu alimwambia anafanya kosa kubwa ambalo atajutia maisha yake yote
5: wakati anaanzisha Amazon hakuwa na uhakika wa anafanya nini
Kabla ya kampuni yake kuitwa Amazon, aliita cadabra, baadaye akaona halifai Baadaye ndiyo aliamua kuchagua Amazon, jina la mto mrefu zaidi akiwa na maono ya kampuni kuwa kubwa zaidi.
6: Amewekeza kwenye makampuni mengine zaidi ya 40
Bezos amekuwa mwekezaji mkubwa kwenye makampuni mengine kama google, Twitter, uber nk Alikuwa mwekezaji wa kwanza kabisa kuwekeza kwenye kampuni ya google kabla hata haijajulikana,aliwekeza dola 250, 000 mwaka 1998.
Wakati huo hisa moja ya google ilikuwa dola 0.04.
Sasa hivi hisa moja ya google inathamani ya dola 966.
Hii ina maana kama hakuuza hisa zake dola laki mbili na nusu aliyowekeza mwaka 1998, sasa hivi imefikia dola bilion sita
7: Anampango wa kuwaondoa binadamu duniani
Lakini siyo kwa kuwaangamiza, bali kwa kuwawezesha kuishi kwenye sayari nyingine .
Kupitia kampuni yake ya Blue origin aliyoianzisha mwaka 2000, anataka watu kwenda sayari nyingine iwe rahisi na nafuu kama watu wanavyosafiri kwenda nchi nyingine
NYONGEZA: Nafasi Bezos kuwa tajiri namba moja duniani ili dumu kwa muda mfupi baada ya thamani za hisa zake kushuka. Hii ili pelekea kuwa mtu tajiri namba mbili duniani,namba moja akiwa Bill Gatess.
Maoni
Chapisha Maoni