Yehova aliwapa wanadamu dunia. Dunia ni makao yetu. Kwa hiyo wanadamu wa kwanza, Adamu na hawa, hawakuumbwa waijaze mbingu kwa kuwa tayari mungu alikuwa amewaumba malaika waishi mbinguni ( ayubu 38:4,7 ) Badala yake mungu alimweka mwanadamu wa kwanza ktk paradiso yenye kupendeza iliyoitwa bustani ya Edeni ( mwanzo 2:15,17 ) yehova alimpa adamu na watoto ambao angepata tumaini la kufurahia maisha duniani milele ( zaburi 37:29, 115:16 ) mwanzoni, bustani ya Edeni tu ndiyo iliyokuwa paradiso wanadamu hao wa kwanza walipaswa kuzaa na kuijaza dunia.
Baada ya muda, wangeitiisha dunia nzima na kuifanya kuwa paradiso ( mwanzo 1:28 ) dunia haitaharibiwa kamwe.
Kwa nini dunia si paradiso leo
Adamu na hawa hawakumtii mingu, hivyo yehova akawafukuza kutoka ktk bustani hiyo. Paradiso ikapotea na hakuna mtu ambaye amefanikiwa kuirudisha.
Biblia inasema dunia imetiwa mkononi mwamwovu ( ayubu 9:24 ) ( mwanzo 3:23,24 )
Je, yehova ameshindwa kutimiza kusudi lake la awali kuelekea wanadamu hapana yeye ni mweza yote hawezi kushindwa ( isaya 45: 18 ) Atawarudisha wanadamu ktk hali ambayo alikusudia wawe nayo ( zaburi 37:11:34 )
Paradiso itarudishwa jinsi gani
Paradiso itarusishwa duniani yesu atakapotawala akiwa mfalme aliyewekwa na mungu.
Ktk vita vinavyoitwa Har magedoni, yesu atawaongoza malaika wa mungu kuwaharibu wote wanaompinga mungu kisha yesu atamfunga shetani kwa miaka 1000.
Watu wa mungu wataokoka uharibifu huo kwa sababu yesu atawalinda na kuwaongoza.
Watafurahi uzima wa milele ktk paradiso duniani ( ufunuo 20:1,3, 21: 3,4 )
Kuteseka kutaisha lini
Mungu ataondoa uovu dunia lini ??
yesu alitoa ishara ya kuonyesha wakati ambapo mwisho ungekuwa karibu.
Hali zilizo ulimwenguni leo zinahatarisha maisha ya watu na zinaonyeaha kwamba tunaishi katika umalizio wa mfumo wa mambo ( mathayo 24:3,7 ) ( 14:21,22 )
Wakati wa utawala wa miaka 1,000 wa yesu atakapo kuwa akiitawala dunia kutoka mbinguni, atakomeaha kuteseka kote ( isaya 9:6, ( isaya 7:11,9 ) zaidi ya kutawala akiwa mfalme yesu atatenda akiwa kuhani mkuu naye atazifuta dhambi za wale wanaompenda mungu hivyo, kupitia yesu, mungu ataondoa magonjwa, uzee na kifo ( isaya 25: 8 ) ( isaya 33: 24 )
Ni nani watakaoishi ktk paradiso
Ktk jumba la ufalme, utakutana na watu wanao mpenda mungu na wanaotaka kujifunza jinsi wanavyo weza kumpendeza watu wanaomtii mungu wataishi katika Paradiso ( 1yohana 2:17 ) yesu aliwatuma wafuasi wake wawatafute watu wapone na kufundisha jinsi ya kuwa watu wenye kukubalika mbele za mungu.
Leo yehova anawatayarisha mamilioni ya watu kuishi ktk paradiso ijayo hapa duniani ( sefania 2:3 ) ( mika 4:1,4 ) amin
Maoni
Chapisha Maoni