Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico.
Kwa upande wa Afrika nchi zinazo lima ni kama malawi, Zimbia na Botswana.
Zao hili hulimwa pia katika nchi za afrika mashariki ikiwemo kenya,uganda na tanzania.
Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania.
Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 Ikiwakilisha asilimia 51 ya mazao yote ya mboga.
Kwa mujibu wa wizara ya kilimo ya tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na mkoa wa kilimanjaro ( Hai, moshi na Rombo ) Arusha ( Arumeru ) Morogoro ( Mgeta ) Tanga ( Lushoto ) Mbeya ( Mbeya Vijijini ) na Singida.
Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 ( ekari 15, 398 ) pamoja na kwamba eneo la uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.
Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, Upepo, Joto, Ukame.
Aina za nyanya
Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika ktk makundi mawili.
a: Aina ndefu ( inter mediate ) kwa mfano ANNA FI, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya green house.
Uvunaji wake ni wa muda mrefu, Zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
b: Aina fupi ( determinate ) kwa mfano Tanya, cal, mwaga, onyx, Roma VF ( nyanya mshumaa ) kutokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi
1: OPV ( open pollinated Variety ) Aina za kawaida
2: Hybrid - chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima l, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana na zanye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.
Kuandaa kitalu cha nyanya mambo muhimu ya kuzingatia
__ Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
__ Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
__ Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmonyoka wa udongo
__ Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo ( au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k )
__ Kiwe sehemu ambayo ni urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine
Kuandaa matuta ya kusia mbegu za nyanya Aina ya matuta:
__ Matuta ya makingo ( sunken seed bed )
__ Matuta ya kunyanyulia udongo ( raised seed bed )
__ Matuta ya kawaida ( flat seed beds )
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuandaa matuta
. Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ Ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyanga miche ]
. Kwatua / lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini
. Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu
. Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/ vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vinzuri na udongo
. Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja ( hatua moja ) mraba
. Tuta lisiwe na mabonde mabonde mabonde au mawemawe ambacho yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe.
Faida na hasara za matuta yaliyotajwa hapo juu
1 Matuta ya kunyanyulia udongo ( raised seed beds )
__ Matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
__ Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutoaha kutanuka haraka zaidi
__ Matuta haya hayatuamisho maji kama mengine. Hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara
Hasara
Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama haya kutengenezwa vinzuri.
2: matuta ya makingo ( sunken seed beds ) faida:
__ Matuta haya ni raisi kutengeneza
__ Hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
__ Nyevu mdogo unaopatikana ardhini
__ Ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
__ Huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
__ Huzuia mmonyoko wa ardhi
Hasara
Matuta ya aina hii hayanawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.
3: matuta ya kawaida ( Flat seed beds )
Faida
__ Ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa na kusambazwa mbegu huoteshwa
__ Ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu
Hasara
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi
Kusia mbegu
__ Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni ( Germination test )
__ Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
Asante sana kwa kusoma nakala hii Tuta endelea wakati mwingine "ASANTE SANA"
Maoni
Chapisha Maoni