Tofauti ktk mahusiano ni jambo ambalo halikwepeki na hakuna mahusiano yasiyo kuwa na tofauti
Pindi watu waliokatika mahusiano wanapotofautiana ni bora wakazijua kanuni hizi
1: watambue neno SAMAHANI halina jinsi Aliyekosea ndiye aombe kusamehewa hili halijalishi ni mme au mke ubabe ktk mahusiano si njia bora ya kumaliza tofauti zenu
2: Tabia ya kususa susa siyo nzuri wengine wakisha tofautiana hususa wakidhani ndio wanatatua tofauti zao wengine hususa kuongeza wengine hususa kula na mbaya zaidi
3: Ugomvi unaoanzia chumbani uishie chumbani huko huko ma usitoke nje. Walio ktk mahusiano wajitahidi kusikiliza na kutatua tofauti zao wenyewe na zaidi kitandani kiwe jukwaa la upatanishi na siyo vinginevyo
4: Mmoja lazima akubali kuumia ili mwenzie apate amani
__ Jifunze kushuka ( some times caln down ) hii itakusaidia kurejesha amani ktk mahusiano yako usipandishe sauti wakati unamwona mwenzio naye yuko juu na kajawa na hasira, kwa kujishusha amani itarejea tu.
5: Acha mawazo ya kuachika
Huyo mi wako zaidi waza urejesho na siyo uharibifu. Mkubaliane mkapatana na mkayaanzisha mahusiano. Usivunje mahusiano uliyoyajenga kwa muda na gharama kubwa kwa jambo dogo sana. Talaka haijawahi kumwacha mtu salamaa.
6: Samehe
Achilia na mchukulie mwenzio hakuna aliye mkamilifu ktk dunia hii. Sisi wote tuna madhaifu ( weekness ) unapoona mahusiano yamedumu ujue hao wamefuzu kiwango cha juu. Kuvumiliana na kuchukuliana
7: Jenga utaratibu wa kufanya ibada pamoja
__ Sote tunajua mpatanishi mkuu ni mwenyenzi mungu. Hivyo mnapounganisha mikono yenu kwa pamoja na mkamuita mungu awasaidie hakika mtakuwa sehemu salama kuliko ukifanya vinginevyo mahusiano yanayotegemea mungu huwa hayateteleki.
Asante sana.
Maoni
Chapisha Maoni