Korea kaskazini kama nchi ya pekee ni tokeo la ugawaji wa korea baada ya vita kuu ya pili ya dunia.
Korea ilikuwa koloni la japan kuanzia 1910 hadi mwaka 1945.
Kwenye mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia jeshi la urusi liliwafuata wa japani kaskazini mwa rasi na wamerekani waliingia kusini mwanzoni kulikuwa na majadiliano ya kuunganisha korea tena.
Lakini vita Baridi ilileta uadui kati ya pande hizo mbili.
Kila moja ilianzisha serikali ya pekee katika kanda la utawala wake kufuatana na itikadi yake warusi walitaifisha tasnia na ardhi wakaacha serikali ya kikomunisti katika kaskazini na wa marekani waliacha uchumi wa kibepari na serikali iliyochaguliwa katika kusini kaika vita ya korea iliyofuata korea ya kaskazini iliweza kudumu kwa sababu ya msaada wa kijeshi wa china iliyomwaga askari milioni moja nchini.
Kiongozi mkomunisti kim ll-sung alishika mamlaka akutawala kama dikteta kwa msaada wa chama cha kikomunisti na jeshi.
Alipokufa mwaka 1994 mwana wake kim jong-ll alichukua nafasi yake hadi alipofariki tarehe 17 Des 2011.
Nafasi yake ilichukuliwa na mtoto wake kim jong-un.
Kim ll-sung aliunda itikadi ya " juche " inaitwa falsafa ya kuendeleza umaksi, lakini hali halisi ni itikadi inayotakiwa kutoa msingi kwa utawala wa kidikteta.
Ingawa ilidai kutafuta maendeleo ya kujitegemea, korea kaskazini ilikuwa nchi iliyotegemea msaada kutoka urusi kwa historia yake yote .
Baada ya mwisho wa umoja wa kisovyeti msaada huo ulikwisha na korea kaskazini iliingia katika kipindi kigumu sana kiuchumi.
Leo hii nchi haiwezi kulisha watu wake hutegemea usaidizi wa vyakula kutoka jumuiya ya kimataifa.
Udikteta katika korea kaskazini ni wa kikomunisti kwa jina lakini una tabia za kidini ndani yake.
Km ll -sung alitangazwa kuwa " rais wa milele " kim ll - sung hakutumia cheo rasmi isipokuwa " mwenyekiti wa kamati ya utetezi wa taifa " kinachomaanisha kitu kama " mkuu wa jeahi " katika mwaka 2006 korea kaskazini ililitekeleza mlipuko wa nyuklia
Miji mkuu
Mji mkuu ni pyongyang asilimia 16 za taifa huishi ktk mji mkuu.
Mji mikubwa mingine haipitiki nusu milioni ya wakazi.
Watu wa korea kaskazini hawawezi kuhama kwa hiari yao kutoka mahali pamoja kwenda penginepo bila kibali
Uchumi
Uchumi wa pande zote mbili za korea ulikuwa duni sana baada ya vita kuu ya pili.
Mwanzoni nchi ilifuata mfano wa kutunga mipangono ya miaka mitano kama umoja wa kisovyeti ( urusi ) viwanda, maduka na biashara yote vilitaifishwa na kuwekwa mkononi mwa dola.
Siasa ili lenga hali ya kujitegemea na biashara ya nje ilitekelezwa tu na nchi za kikomunisti.
Pamoja na maendeleo ya haraka ya kiuchumi hadi mnamo 1960.
Hapo tija ya mfumo wa uchumi unaopangwa ulianza kufikia mwisho wake na kuonyesha upungufu wa nguvu kazi, ardhi ya kulima na vyombo vya usafiri na malengo ya mipango haya kufikiwa tena kuanzia 1980 korea kusini ilianza kupita mafanikio ya uchumi wa kaskazini.
Mwaka 1993 korea kaskazini iliacha kutangaza mipango ya uchumi
Maoni
Chapisha Maoni