Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Biblia inasema nini mwisho wa dunia utkuja lini Na Wilson Mtishbi

Mwisho utakuja wakati wanadamu watakapokuwa wameonywa kikamili kupitia kazi ya ulimwenguni pote ya kutangaza ufalme wa mungu. Ufalme huo ni serikali itakayotawala dunia nzima wakati ambapo serikali za wanadamu zitaondolewa ( daniel 7:13,14 ) yesu kristo alisema hivi " hii habari njema ya ufalme itahubiriwa katika dunia yote na inayokaliwa ili kuwa ushahidi kwa mataifa yote na ndipo ule mwisho utakapokuja ( mathayo 24:14 ) kazi hiyo ya kuhubiri, inayoonyesha haki na rehema ya mungu ni sehemu ya ishara yenye mambo mengi ya siku za mwisho ishara hiyo inatia ndani pia vita kati ya mataifa matetemeko ya inchi, njaa, na magonjwa ( mathayo 24:3 ) ( luka 21:10,11 ) mbali na kutabiri matukio ya ulimwengu Biblia inatueleza pia kuhusu mabadiliko ya kijamii katika siku za mwisho inasema hivi kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe wenye kupenda pesa wasiotii wazazi wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema, wanaopenda raha badala ya kumpenda mungu ( 2 Timotheo 3:1,5 ) ulimwengu huu mwovu karibuni utapitilia mbali ( 1 yohana 2:17 ) hali hizo zina tambulisha kipindi kilichoanza mwaka 1914 hivi, wakati wa vita vya kwanza vya ulimwengu.
" kwa hiyo, endeleeni kukesha kwa sababu hamwijui ile siku wala saa " ( mathayo 25 :13 )

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.

Fahamu jinsi ya kutengeneza sabuni ya vyoo

Sabuni ya kusafisha vyoo Malighafi. 1. Sulphonics Acid Lita 1 2. Soda Ash nusu 1/2 kilo 3. Sless 4. Chumvi 1/2 kilo 5. Maji lita 17 1/2 _ 20 6. Rangi kijani 7. Pafyumu 8. Formalin Jinsi ya kutengeneza Weka maji lita 5 kisha anza kukoroga, ongeza lita 5 kisha lita 5 tena na mwisho lita 2 4. Chumvi 1/2 kg 3. Sless nusu lita 2. Soda ash nusu kilo 1. Sulphonics Acid lita 1 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu ni vinzuri kuweka kwenye ndoo lita 10 ya sabuni utaweka rangi kijiko 1 cha chai, rangi ya kijani pafyumu aina ya ' Rose two one ' au pino vijiko 5 vya chakula na Formalin vijiko 3 vya chakula. Formalin kwa ajili ya kuua wadudu ( bacteria ) ni vinzuri sana kuwemo kwenye sabuni ya chooni kwani ina kazi nyingi zaidi ya hiyo iliyotajwa Asante sana rafiki sasa chukua hatua ya kufanya hakika utafanikiwa sana

Somo: Roho mtakatifu Na mwl Christopher Mwakasege

Kushirikiana Na Roho Mtakatifu Anapotumia Moto kukuongoza ili utembee kwenye mapenzi ya mungu Biblia inafundisha ya kuwa wana wa mungu huwa wanaishi na wanatakiwa waishi kwa kuongozwa na roho mtakatifu ( warumi 8 : 14, 16, 17 ) Njia moja wapo anayotumia roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa mungu, ni kwa kutumia moto wa mungu anaokuja nao ndani ya mtu anapoingia kukaa kwake Biblia inasema juu ya yesu ya kuwa yeye atawabatiza kwa roho mtakatifu na kwa moto ( luka 3 : 16 ) na siku ya pentekoste, wakati wanafunzi wa kwanza wa yesu, walipokuwa wamekutanika pamoja kukuwatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao wote wakajazwa roho mtakatifu ( matendo 2 : 3,4 ) Unaposoma na kutafakari jambo lililotokea siku hiyo ya pentekoste, utajua kuwa kuna uhusiano kati ya ndimi za moto juu ya kila mmoja wao na kule kujazwa roho mtakatifu kwa kila mmoja wao ni dhahiri ya kuwa roho mtakatifu anaingia ndani ya kila mwana wa mungu akiwa pia na moto wa mungu pamoja nao kazi m...