Mwili wa mnyama siyo mkavu kama vile jiwe. Mwili una majimaji. Mifupa huonekana mikavu. Lakini kwa kweli ina kiasi fulani cha maji Tukisikia kiu tunakunywa maji. Kiu ni ishara ya jambo gani? Tukisikia kiu maana yake maji yamepungua mwilini. Hivyo, kila wakati mwili unahitaji kuwa na maji kiasi fulani. Kwa nini mwili unahitaji maji? Mwili ni lazima ufanyr kazi zake za ndani ambazo ni za muhimu kwa uhai. Kazi hizo haziwezi kutendeka bila kuwepo maji. Hivyo bila maji hakutakuwa na uhai.